1 Timothy 1:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waambie waachane na zile hadithi tupu na orodha ndefu za mababu, ambazo huleta tu ubishi, wala haviwajengi watu katika mpango ujulikanao kwa imani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si madaraka ya Mungu yaliyo katika imani; basi ufanye hivyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Uwaambie wasitumie muda wao kusimulia simulizi zisizo na maana za mambo ya kale na kutengeneza orodha ndefu ya mababu. Mambo hayo husababisha mabishano tu na hayaisaidii katika kuikamilisha kazi ya Mungu tuliyopewa, ambayo ni lazima tuikamilishe kwa imani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Waambie waachane na zile hadithi tupu na orodha ndefu za mababu, ambazo huleta tu ubishi, wala haviwajengi watu katika mpango ujulikanao kwa imani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waambie waachane na zile hadithi tupu na orodha ndefu za mababu, ambazo huleta tu ubishi, wala haviwajengi watu katika mpango ujulikanao kwa imani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha zisizo na mwisho za majina ya vizazi ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Kimungu utokanao na imani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na kikomo, zinazozua maswali wala si mpango wa Mungu ulio katika imani; basi uwaambie hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waambie waachane na zile hadithi tupu na orodha ndefu za mababu, ambazo huleta tu ubishi, wala haviwajengi watu katika mpango ujulikanao kwa imani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wala wasishikamane na masimulio yasiyo ya kweli wala na mambo ya mashina ya koo za kale yasiyokoma. Haya huleta mabishano, lakini hayaufalii utunzaji wa Mungu wa kuwatunza wenye kumtegemea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si madaraka ya Mungu yaliyo katika imani; basi ufanye hivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie wasishikamane na hadisi za uongo, pamoja na mambo yasiyokuwa na mwisho ya wababu. Hayo yote yanaleta mabishano, wala hayafai kitu kwa kutimiza mupango wa Mungu wa wokovu, unaojulikana kwa njia ya imani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si ujenzi wa Mungu ulio katika imani; bassi sasa nakuagiza vivyo hivyo.