1 Timothy 1:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanapenda kuwa waalimu wa sheria, lakini hawaelewi maneno yao wenyewe au mambo wanayosisitiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wanataka kuwa walimu wa Torati, lakini hawajui mambo yale wanayosema wala hayo wanayoyatumainia kwa uthabiti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wapenda kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wanataka kuwa walimu wa sheria, lakini hawafahamu mambo wanayosema, wanasema kwa ujasiri wote juu ya mambo wasiyoyaelewa wenyewe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wanapenda kuwa walimu wa Sheria, lakini hawaelewi maneno yao wenyewe au mambo wanayosisitiza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanapenda kuwa waalimu wa sheria, lakini hawaelewi maneno yao wenyewe au mambo wanayosisitiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wanataka kuwa walimu wa sheria, lakini hawajui mambo yale wanayosema wala hayo wanayoyatumainia kwa uthabiti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wanataka kuwa walimu wa Torati, lakini hawajui mambo yale wanayosema wala hayo wanayoyatumainia kwa uthabiti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakitaka kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanapenda kuwa waalimu wa sheria, lakini hawaelewi maneno yao wenyewe au mambo wanayosisitiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
walitaka kuwa wafunzi wa Maonyo, lakini hawajui, wala wasemayo, wala wabishayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wapenda kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanataka kuwa walimu wa Sheria ya Musa, lakini hawaelewi wao wenyewe maneno wanayosema wala maneno wanayohakikisha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wapenda kuwa waalimu wa sharia, wasiyafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa utbabiti.