1 Timothy 1:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba sheria haziwekwi kwa ajili ya watu wema, bali kwa ajili ya wahalifu na wasiotii, wasiomcha Mungu na wenye dhambi, watu wasio na dini na wa kidunia, watu wanaowaua baba na mama zao, au wauaji wowote wale;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini tunajua ya kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, kwa ajili ya wasiomcha Mungu na wenye dhambi, wasio watakatifu na wanaokufuru; kwa wale wawauao baba zao au mama zao, kwa wauaji,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia tunajua kwamba sheria haikutengenezwa kwa ajili ya wale wanaotenda haki. Imetengenezwa kwa ajili ya wale wanayoipinga na kukataa kuifuata. Sheria ipo kwa ajili ya wenye dhambi wanaompinga Mungu na mambo yote yanayompendeza. Ipo kwa ajili ya wale wasio na hamu ya mambo ya kiroho na kwa ajili ya wale wanaowaua baba au mama zao au mtu yeyote yule.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba sheria haziwekwi kwa ajili ya watu wema, bali kwa ajili ya wahalifu na wasiotii, wasiomcha Mungu na wenye dhambi, watu wasio na dini na wa kidunia. Watu wanaowaua baba na mama zao, au wauaji wowote wale;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba sheria haziwekwi kwa ajili ya watu wema, bali kwa ajili ya wahalifu na wasiotii, wasiomcha Mungu na wenye dhambi, watu wasio na dini na wa kidunia, watu wanaowaua baba na mama zao, au wauaji wowote wale;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini tunajua ya kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, kwa ajili ya wasiomcha Mungu na wenye dhambi, wasio watakatifu na wanaokufuru, kwa wale wawauao baba zao au mama zao, kwa wauaji,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini tunajua ya kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, kwa ajili ya wasiomcha Mungu na wenye dhambi, wasio watakatifu na wanaokufuru; kwa wale wawauao baba zao au mama zao, kwa wauaji,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu asiye na hatia, bali wavunjao sheria, waasi, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba sheria haziwekwi kwa ajili ya watu wema, bali kwa ajili ya wahalifu na wasiotii, wasiomcha Mungu na wenye dhambi, watu wasio na dini na wa kidunia, watu wanaowaua baba na mama zao, au wauaji wowote wale;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwa kujua kwamba: Mwongofu siye aliyetolewa Maonyo, ila waliotolewa ndio wapotovu nao wasiotii nao wasiomcha Mungu nao wakosaji nao wachafu nao wabezi nao wauao baba zao nao wauao mama zao nao wauao wenzao
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile ni sherti kujua kwamba Sheria haikuwekwa kwa ajili ya wenye haki, lakini kwa ajili ya watenda mabaya, waasi, watu wasiomuheshimu Mungu, wenye zambi, nao wenye kuchafua vitu vitakatifu na kukufuru, na kwa ajili ya wale wanaowaua wababa zao au wamama zao, na wauaji wowote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nawe ufahamu neno hili, ya kuwa sharia haimkhusu mtu wa haki, bali maasi, mi wasio taratihu, na makafiri, na wenye dhambi, na wasio watakatifu, na wasiomcha Mungu, na wauao baba zao, na wauao mama zao, mi wauaji,