1 Timothy 2:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mwanamke ataokolewa kwa kuzaa kwake, wakiendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kuwa na kiasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini wanawake wataokolewa kwa jukumu lao la kuzaa watoto. Wakiendelea kuishi katika imani, upendo, utakatifu na tabia njema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mwanamke ataokolewa kwa kuzaa kwake kama wakiendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kuwa na kiasi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mwanamke ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakiendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kuwa na kiasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ataokoka kwa kuzaa watoto, hao wakiwa wenye kumtegemea Mungu na wenye kupendana na wenye kutakaswa mioyo na wenye kuonyeka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa hivi mwanamuke ataokolewa kwa kuzaa watoto, kama akidumu katika imani, upendo na utakatifu na kuwa mukadirifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini ataokolewa, kwa ule uzazi, kama wakidumu katika imani na npendo na utakatifu pamoja na moyo wa kiasi.