1 Timothy 2:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu hiyo mimi nilitumwa niwe mtume na mwalimu wa watu wa mataifa, niutangaze ujumbe wa imani na ukweli. Nasema ukweli; sisemi uongo!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami kwa kusudi hili nimewekwa niwe mhubiri na mtume (nasema kweli katika Al-Masihi wala sisemi uongo), mwalimu wa watu wa Mataifa katika imani na kweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nami nilichaguliwa kama mtume kuwaambia watu ujumbe huo. Ninasema kweli. Sidanganyi. Nilichaguliwa kuwafundisha wasio Wayahudi na nimefanya kazi hii kwa imani na ukweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa sababu hiyo mimi nilitumwa niwe mtume na mwalimu wa watu wa mataifa, niutangaze ujumbe wa imani na ukweli. Nasema ukweli; sisemi uongo!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu hiyo mimi nilitumwa niwe mtume na mwalimu wa watu wa mataifa, niutangaze ujumbe wa imani na ukweli. Nasema ukweli; sisemi uongo!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami kwa kusudi hili nimewekwa niwe mhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo wala sisemi uongo), mwalimu wa watu Mataifa katika imani na kweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami kwa kusudi hili nimewekwa niwe mhubiri na mtume (nasema kweli katika Al-Masihi wala sisemi uongo), mwalimu wa watu wa Mataifa katika imani na kweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami kwa ajili ya huo niliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu hiyo mimi nilitumwa niwe mtume na mwalimu wa watu wa mataifa, niutangaze ujumbe wa imani na ukweli. Nasema ukweli; sisemi uongo!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nimewekewa kuwa mtangazaji na mtume wake, nasema kweli, sisemi uwongo, niwe mfunzi wa wamizimu, niwafundishe kumtegemea Mungu na kuyashika yaliyo ya kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni kwa hiyo nimewekwa kuwa mujumbe na mutume kwa kuwafundisha watu wa mataifa mengine kusudi wapate kumwamini Mungu na kutambua ukweli. Mimi ninasema ukweli wala si uongo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli.