1 Timothy 3:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wake zao wanapaswa pia kuwa na tabia njema, wasiowasengenya watu, wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo, wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasio wasingiziaji, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa njia hiyo hiyo wanawake wanaoteuliwa kuwa mashemasi wanapaswa kuwa wale wanaoastahili kuheshimiwa. Wasiwe wanawake wanaosema mambo mabaya juu ya watu wengine. Ni lazima wawe na kiasi. Ni lazima wawe wanawake wanaoweza kuaminiwa kwa kila jambo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wake zao wanapaswa pia kuwa na tabia njema, wasiowasengenya watu, wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wake zao wanapaswa pia kuwa na tabia njema, wasiowasengenya watu, wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo, wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasiozungumza maneno ya kuwadhuru wengine, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo, wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasio wasingiziaji, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; wasiwe wachongezi; ila wawe watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wake zao wanapaswa pia kuwa na tabia njema, wasiowasengenya watu, wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vivyo hivyo nao wake zao wawe wenye macheo wasiosengenya, wasiokunywa kileo, walio waelekevu katika mambo yote!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanawake wao wanapaswa kuwa na adabu vilevile, wasikuwe wasingiziaji wa uongo, lakini wakuwe wakadirifu na waaminifu katika mambo yote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Vivi hivi wanawake wawe watu wa utaratibu, si wasingiziaji, watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.