1 Timothy 3:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana wasaidizi wanaofanya kazi yao vizuri hujipatia msimamo mzuri, na wanaweza kusema bila hofu juu ya imani yao katika Kristo Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale ambao wamehudumu vyema katika huduma ya ushemasi hujipatia msimamo bora na ujasiri mkubwa katika imani yao ndani ya Al-Masihi Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mashemasi wanaofanya kazi yao vyema wanajitengenezea nafasi nzuri ya kuheshimiwa. Nao kwa kiasi kikubwa sana wanajihakikishia imani yao katika Kristo Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana wasaidizi wanaofanya kazi yao vizuri hujipatia msimamo mzuri, na wanaweza kusema bila hofu juu ya imani yao katika Kristo Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana wasaidizi wanaofanya kazi yao vizuri hujipatia msimamo mzuri, na wanaweza kusema bila hofu juu ya imani yao katika Kristo Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale ambao wamehudumu vyema katika huduma ya ushemasi hujipatia msimamo bora na ujasiri mkubwa katika imani yao ndani ya Kristo Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale ambao wamehudumu vyema katika huduma ya ushemasi hujipatia msimamo bora na ujasiri mkubwa katika imani yao ndani ya Al-Masihi Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana watendao vema kazi ya ushemasi hujipatia daraja zuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana wasaidizi wanaofanya kazi yao vizuri hujipatia msimamo mzuri, na wanaweza kusema bila hofu juu ya imani yao katika Kristo Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani waliotumika vizuri hujipatia fungu zuri, tena kwa hivyo, wanavyomtegemea Kristo Yesu, huona furaha nyingi kwa kumtangaza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wasaidizi wanaotumika vizuri kazi zao, wanajiheshimisha, na wanaweza kutangaza kwa uhodari habari za imani tunayokuwa nayo katika kuungana na Kristo Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana watendao kazi ya ushemasi vema hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.