1 Timothy 3:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama nikicheleweshwa, basi, barua hii itakufahamisha mwenendo tunaopaswa kuwa nao katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai, na ambalo ni nguzo na msingi wa ukweli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nikikawia, utajua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambayo ndiyo jumuiya ya waumini ya Mungu aliye hai, iliyo nguzo na msingi wa kweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
ili kwamba, hata kama sitakuja mapema, utafahamu jinsi ambavyo watu wanapaswa kuishi katika familia ya Mungu. Familia hiyo ni kanisa la Mungu aliye hai. Na Kanisa la Mungu ni msaada na msingi wa ukweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kama nikicheleweshwa, basi, barua hii itakufahamisha mwenendo tunaopaswa kuwa nao katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai, na ambalo ni nguzo na msingi wa ukweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama nikicheleweshwa, basi, barua hii itakufahamisha mwenendo tunaopaswa kuwa nao katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai, na ambalo ni nguzo na msingi wa ukweli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama nikikawia, utajua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambayo ndiyo kanisa la Mungu aliye hai, lililo nguzo na msingi wa kweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama nikikawia, utajua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambayo ndiyo jumuiya ya waumini ya Mungu aliye hai, iliyo nguzo na msingi wa kweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama nikicheleweshwa, basi, barua hii itakufahamisha mwenendo tunaopaswa kuwa nao katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai, na ambalo ni nguzo na msingi wa ukweli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama nakawia, ujue mwenendo unaopasa katika nyumba ya Mungu! Hiyo nyumba ndio wateule wake Mungu aliye Mwenye uzima; nao ndio nguzo na msingi wa kuyashikiza yaliyo ya kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, kama nikikawia kufika, utaweza hivi kujua mwenendo unaopaswa kuwa nao katika nyumba ya Mungu, maana yake katika jamaa ya Mungu Mwenye Uzima. Yeye ndiye anayekuwa nguzo na musingi wa kweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini nikikawia, upate kujua sana jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu iliyo kanisa la Mungu aliye hayi, nguzo na msingi wa kweli.