1 Timothy 3:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri ya dini yetu: Alionekana katika umbo la kibinadamu, alithibitishwa na Roho kuwa ni mwadilifu, akaonekana na malaika. Alihubiriwa kati ya mataifa, aliaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bila shaka yoyote, siri ya utauwa ni kubwa: Alidhihirishwa katika mwili, akathibitishwa kuwa na haki katika Roho wa Mungu, akaonekana na malaika, akahubiriwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, Mungu ametuonesha siri ya maisha yanayompa heshima na kumpendeza Yeye. Siri hii ya ajabu ni ukweli ambao wote tunakubaliana nao: Kristo alijulikana kwetu katika umbile la kibinadamu; alioneshwa na Roho kuwa kama alivyojitambulisha; alionwa na malaika. Ujumbe kuhusu Yeye ulitangazwa kwa mataifa; watu ulimwenguni walimwamini; alichukuliwa juu mbinguni katika utukufu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri ya dini yetu: Alionekana katika umbo la kibinadamu alithibitishwa na Roho kuwa ni mwadilifu, akaonekana na malaika. Alihubiriwa kati ya mataifa, aliaminiwa popote ulimwenguni, akachukuliwa juu mbinguni katika utukufu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri ya dini yetu: Alionekana katika umbo la kibinadamu, alithibitishwa na Roho kuwa ni mwadilifu, akaonekana na malaika. Alihubiriwa kati ya mataifa, aliaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bila shaka yo yote, siri ya utauwa ni kubwa: Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, akathibitishwa kuwa na haki katika Roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bila shaka yoyote, siri ya utauwa ni kubwa: Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, akathibitishwa kuwa na haki katika Roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri ya dini yetu: Alionekana katika umbo la kibinadamu, alithibitishwa na Roho kuwa ni mwadilifu, akaonekana na malaika. Alihubiriwa kati ya mataifa, aliaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli fumbo lililo kuu ni lile la kumcha Mungu: Mungu alitokea waziwazi mwilini, akapata wongofu kwa kuwa mwenye Roho, akaonekana penye malaika, akatangazwa kwa wamizimu, akategemewa ulimwenguni, akapazwa mbinguni kwenye utukufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakika siri ya ibada yetu ni kubwa: Yeye alitokea kwa mufano wa mutu, alishuhudiwa na Roho Mutakatifu kuwa mwenye haki. Alionekana na wamalaika. Alitangazwa katikati ya mataifa. Aliaminiwa popote katika dunia. Na alinyanyuliwa mbinguni katika utukufu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.