1 Timothy 3:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Anapaswa awe mwenye sifa njema kati ya watu walio nje ya kanisa, ili asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa Ibilisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Inampasa pia awe na sifa njema kwa watu walio nje, ili asije akalaumiwa na kuanguka kwenye mtego wa ibilisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia, ni lazima askofu aheshimiwe na watu walio nje ya Kanisa. Kwa namna hiyo hataweza kukosolewa na kuabishwa na wengine na kunasa kwenye mtego wa Shetani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Anapaswa awe mwenye sifa njema kati ya watu walio nje ya kanisa, ili asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa Ibilisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Anapaswa awe mwenye sifa njema kati ya watu walio nje ya kanisa, ili asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa Ibilisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Inampasa pia awe na sifa njema kwa watu walio nje, ili asije akalaumiwa na kuanguka kwenye mtego wa ibilisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Inampasa pia awe na sifa njema kwa watu walio nje, ili asije akalaumiwa na kuanguka kwenye mtego wa ibilisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Anapaswa awe mwenye sifa njema kati ya watu walio nje ya kanisa, ili asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa Ibilisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao walioko nje sharti wamshuhudie kuwa mwema, asije kusingiziwa mabaya, akanaswa na tanzi la Msengenyaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile inafaa akuwe mutu mwenye kushuhudiwa vizuri na watu wa inje ya kanisa, kusudi asizarauliwe na kunaswa katika mutego wa Shetani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Imempasa tena kushuhudiwa mazuri na watu walio nje; asitumbukie katika lawama na mtego wa Shetani.