1 Timothy 3:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wasaidizi katika kanisa wanapaswa pia kuwa watu wenye tabia njema na wanyofu; wasiwe wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo, mashemasi nao wawe watu wanaostahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili au wenye kujifurahisha kwa mvinyo, wala wanaotamani faida isiyo halali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vivyo hivyo mashemasi
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa njia hiyo hiyo, watu wanaoteuliwa kuwa mashemasi inawapasa kuwa wale wanaostahili kuheshimiwa. Wasiwe watu wanaosema mambo wasiokuwa nayo moyoni au wanaotumia muda wao mwingi katika ulevi. Wasiwe watu wanaowaibia fedha watu wengine kwa udanganyifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wasaidizi katika kanisa wanapaswa pia kuwa watu wenye tabia njema na wanyofu; wasiwe wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wasaidizi katika kanisa wanapaswa pia kuwa watu wenye tabia njema na wanyofu; wasiwe wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo, mashemasi nao wawe watu wanaostahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili au wenye kujifurahisha kwa mvinyo, wala wanaotamani faida isiyo halali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo, mashemasi nao wawe watu wanaostahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili au wenye kujifurahisha kwa mvinyo, wala wanaotamani faida isiyo halali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wasaidizi katika kanisa wanapaswa pia kuwa watu wenye tabia njema na wanyofu; wasiwe wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vivyo hivyo nao watumikiaji wa wateule wawe wenye macheo, wasiosema kuwili, wasio walewi, wasiofuata machumo mabaya,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vivyo hivyo mashemasi 8 na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile wasaidizi wanaotumika katika kanisa wanapaswa kuwa watu wenye heshima. Hawapaswi kuwa wenye nia mbili katika masemi yao wala wenye kunywa pombe kwa uwingi wala wenye kutafuta mali kwa njia isiyokuwa sawa;
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Vivi hivi mashemasi, wawe watu wa utaratibu, si wenye nia mbili, si watu wa kutumia mvinyo nyingi, wawe watu wasiotamani fedha ya aibu;