1 Timothy 4:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usiache kukitumia kile kipaji cha Kristo ndani yako ulichopewa kwa maneno ya manabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Usiache kutumia kipawa kilicho ndani yako, ambacho ulipewa kwa neno la unabii wakati wazee walikuwekea mikono.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kumbuka kutumia kipawa ulichonacho, ambacho ulipewa kupitia unabii wakati kundi la wazee lilipo kuweka mikono juu yako.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Usiache kukitumia kile kipaji cha Kristo ndani yako ulichopewa kwa maneno ya manabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usiache kukitumia kile kipaji cha Kristo ndani yako ulichopewa kwa maneno ya manabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Usiache kutumia kipawa kilicho ndani yako, ambacho ulipewa kwa neno la unabii wakati wazee walipokuwekea mikono.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Usiache kutumia kipawa kilicho ndani yako, ambacho ulipewa kwa neno la unabii wakati wazee walikuwekea mikono.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usiache kukitumia kile kipaji cha Kristo ndani yako ulichopewa kwa maneno ya manabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Usiache kuyatunza yale mema, uliyogawiwa kwa kufumbuliwa kwanza, kisha ukayapata kwa kubandikiwa mikono ya wazee.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usiache kutumia ile zawadi ya kiroho inayokuwa ndani yako, uliyopokea kutokana na maneno ya manabii na kwa njia ya kuwekewa mikono na wazee wa kanisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Usiache kuitumia ile karama iliyo udani yako uliyopewa wewe kwa unabii, na kwa kuwekewa mikono ya wazee.