1 Timothy 4:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama ukiwapa ndugu wote maagizo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, ukijiendeleza kiroho kwa maneno ya imani na mafundisho ya kweli ambayo wewe umeyafuata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukiwakumbusha ndugu mambo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Al-Masihi Isa, uliyelelewa katika kweli ya imani na yale mafundisho mazuri uliyoyafuata.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waambie haya kaka na dada huko. Hii itakuonesha wewe kuwa ni mtumishi mwema wa Kristo Yesu. Utaonyesha kwamba umefundishwa maneno ya imani na mafundisho mazuri uliyoyafuata.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama ukiwapa ndugu wote maagizo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, ukijiendeleza kiroho kwa maneno ya imani na mafundisho ya kweli, ambayo wewe umeyafuata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama ukiwapa ndugu wote maagizo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, ukijiendeleza kiroho kwa maneno ya imani na mafundisho ya kweli ambayo wewe umeyafuata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ukiwakumbusha ndugu mambo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, uliyelelewa katika kweli ya imani na yale mafundisho mazuri uliyoyafuata.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ukiwakumbusha ndugu mambo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Al-Masihi Isa, uliyelelewa katika kweli ya imani na yale mafundisho mazuri uliyoyafuata.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoefu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama ukiwapa ndugu wote maagizo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, ukijiendeleza kiroho kwa maneno ya imani na mafundisho ya kweli ambayo wewe umeyafuata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukiwafundisha ndugu mambo hayo utakuwa mtumishi mzuri wa Kristo Yesu, nawe utajilisha maneno, tuyategemeayo, tunayoyafundisha kwamba: Ni mazuri; ni hayo, uliyoyafuata nawe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama ukiwaelezea waziwazi wandugu maneno hayo, utakuwa mutumishi mwema wa Kristo Yesu, mwenye kukulishwa kiroho na maneno ya imani na mafundisho mazuri uliyoshika kabisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ukiwakumhusha ndugu hayo, utakuwa mkhudumu mwema wa Yesu Kristo, na mzoevu wa maneno ya imani, na ya mafundisho yale mazuri uliyoyafuata.