1 Timothy 4:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mazoezi ya mwili yana faida yake, lakini mazoezi ya kiroho yana faida za kila namna, maana yanatuahidia uhai katika maisha ya sasa, na pia hayo yanayokuja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana mazoezi ya mwili yana faida kwa sehemu, lakini utauwa una faida katika mambo yote, yaani unayo ahadi ya uzima wa sasa na ya ule ujao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kufanya mazoezi ya mwili wako kuna manufaa kidogo kwako. Lakini kujaribu kumpendeza Mungu kwa njia zote kunakufaa zaidi. Kunakuletea baraka katika maisha haya na maisha ya baadaye pia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mazoezi ya mwili yana faida yake, lakini mazoezi ya kiroho yana faida za kila namna, maana yanatuahidia uzima katika maisha ya sasa, na pia hayo yanayokuja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mazoezi ya mwili yana faida yake, lakini mazoezi ya kiroho yana faida za kila namna, maana yanatuahidia uhai katika maisha ya sasa, na pia hayo yanayokuja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana mazoezi ya mwili yana faida kwa sehemu, lakini utauwa una faida katika mambo yote, yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa na ya ule ujao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana mazoezi ya mwili yana faida kwa sehemu, lakini utauwa una faida katika mambo yote, yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa na ya ule ujao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mazoezi ya mwili yana faida yake, lakini mazoezi ya kiroho yana faida za kila namna, maana yanatuahidia uhai katika maisha ya sasa, na pia hayo yanayokuja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mazoezo ya mwili hufalia mambo machache tu; lakini kumcha Mungu hufalia mambo yote, tena kunacho kiago cha uzima wa sasa na cha ule utakaokuwapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mazoezi ya mwili yana mafaa kidogo, lakini kushikamana na ibada kuna mafaa katika mambo yote, kwa maana kunatupatia ahadi ya kuishi kwa wakati huu wa sasa na kwa wakati utakaokuja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jitahidi kupata utawa. Maana, kujitahidi kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, hali utawa hufaa kwa mambo yote; maana nna ahadi ya uzima wa sasa na wa ule utakaokuwa.