1 Timothy 5:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na si kuliachia kanisa mzigo huo, ili kanisa liweze kuwatunza wajane wale waliobaki peke yao kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane katika jamaa yake, inampasa awasaidie wala si kuwaacha wakililemea kundi la waumini, ili lile kundi liweze kuwasaidia wale ambao ni wajane kweli kweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kama yupo mwanamke aliyeamini aliye na wajane katika familia yake, ni lazima awatunze yeye mwenyewe. Ndipo Kanisa halitakuwa na mzigo wa kuwatunza hao bali kuwatunza ambao hawana mtu yeyote wa kuwasaidia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na si kuliachilia kanisa mzigo huo, ili kanisa liweze kuwatunza wajane wale waliobaki peke yao kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na si kuliachia kanisa mzigo huo, ili kanisa liweze kuwatunza wajane wale waliobaki peke yao kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama mwanamke ye yote aaminiye ana wajane katika jamaa yake, inampasa awasaidie wala si kuwaacha wakililemea kanisa, ili kanisa liweze kuwasaidia wale ambao ni wajane kweli kweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane katika jamaa yake, inampasa awasaidie wala si kuwaacha wakililemea kundi la waumini, ili lile kundi liweze kuwasaidia wale ambao ni wajane kweli kweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanamke aaminiye, akiwa na jamaa walio wajane wa kweli, na awasaidie mwenyewe, kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na si kuliachia kanisa mzigo huo, ili kanisa liweze kuwatunza wajane wale waliobaki peke yao kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mwanamke mwenye kumtegemea Mungu akiwa na wajane mwake, na awatunze, wateule wasilemewe, wapate kuwatunza walio wajane kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama mwamini yeyote akiwa na wajane katika jamaa lake, anapaswa kuwasaidia kusudi kanisa lisilemewe. Na hivi kanisa nalo litaweza kuwasaidia wale wajane wasiokuwa na tegemeo lolote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwanamume au mwanamke aamimye, akiwa na wajane, awasaidie, kanisa lisilemewe; illi liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.