1 Timothy 5:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Viongozi wa kanisa wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wazee wa kundi la waumini wanaoongoza shughuli za kundi hilo vizuri wanastahili heshima mara mbili, hasa wale ambao kazi yao ni kuhubiri na kufundisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wazee wanaoliongoza Kanisa katika njia nzuri wanapaswa kupokea heshima mara mbili; hasa wale wanaofanya kazi ya kuhubiri na kufundisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wazee wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Viongozi wa kanisa wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wazee wa kanisa wanaoongoza shughuli za kanisa vizuri wanastahili heshima mara mbili, hasa wale ambao kazi yao ni kuhubiri na kufundisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wazee wa kundi la waumini wanaoongoza shughuli za kundi hilo vizuri wanastahili heshima mara mbili, hasa wale ambao kazi yao ni kuhubiri na kufundisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kutoa unabii na kufundisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Viongozi wa kanisa wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wazee wanaosimamia vizuri sharti wapewe heshima mara mbili, kupita wengine ni wale wanaojisumbua kulitumikia lile Neno kwa kulifundisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazee wa kanisa wanaoongoza kazi yao vizuri wanastahili kupokea mushahara mara mbili, hasa zaidi wale wanaojitolea kwa kufanya kazi ya kuhubiri na kufundisha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.