1 Timothy 5:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika watakatifu, uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninakuagiza mbele za Mungu na mbele za Al-Masihi Isa na mbele za malaika wateule, shika maagizo haya pasipo ubaguzi wala upendeleo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mbele ya Mungu na Kristo Yesu na malaika walioteuliwa, nakuambia fanya hukumu hizo bila upendeleo. Mtendee kila mtu sawa sawa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu, na mbele ya malaika watakatifu uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika watakatifu, uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninakuagiza mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu na mbele za malaika wateule, shika maagizo haya pasipo ubaguzi wala upendeleo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninakuagiza mbele za Mungu na mbele za Al-Masihi Isa na mbele za malaika wateule, shika maagizo haya pasipo ubaguzi wala upendeleo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lolote kwa upendeleo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika watakatifu, uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namtaja Mungu na Kristo Yesu nao malaika waliochaguliwa kuwa mashahidi nikikuagiza sasa, uyashike maneno haya, nalo utakalolifanya lo lote, ulifanye pasipo kuchukizwa wala pasipo kupendezwa na mtu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninakuagiza mbele ya Mungu na mbele ya Kristo Yesu na ya wamalaika watakatifu, ushike kanuni hizo bila kuwazia mutu kitu wala kuwa na upendeleo katika mambo yote unayofanya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Bwana Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, yatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.