1 Timothy 5:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipa wazazi wao na wazee wao, kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hawa inawapasa awali ya yote wajifunze kutimiza wajibu wao wa kumcha Mungu katika matendo kwa kuwatunza wale wa jamaa zao wenyewe, na hivyo wawarudishie wema waliowatendea wazazi wao, kwa kuwa hivi ndivyo inavyompendeza Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mjane akiwa na watoto au wajukuu, jambo la kwanza ambalo wanahitaji kujifunza ni hili: kutimiza wajibu waliyonao kwa wanafamilia wao. Kwa kuwapa heshima na kuwahudumia, watakuwa wanawalipa fadhila wazazi wao na pia mababu na nyanya zao. Na haya ndiyo mambo yanaompendeza Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipa wazazi wao na wazee wao, kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipa wazazi wao na wazee wao, kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hawa inawapasa awali ya yote wajifunze kutimiza wajibu wao wa kumcha Mungu katika matendo, kuwatunza wale wa jamaa zao wenyewe ili wawarudishie wema ule wazazi wao waliowatendea, kwa kuwa hivi ndivyo impendezavyo Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hawa inawapasa awali ya yote wajifunze kutimiza wajibu wao wa kumcha Mwenyezi Mungu katika matendo kwa kuwatunza wale wa jamaa zao wenyewe, na hivyo wawarudishie wema waliowatendea wazazi wao, kwa kuwa hivi ndivyo impendezavyo Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipa wazazi wao na wazee wao, kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mwanamke mjane akiwa na watoto au wajukuu, basi, hao wajifunze kwanza kuwaheshimu walio nao nyumbani mwao wenyewe, wakiwalipa wamama na wabibi mema, walioyapata kwao! Kwani hivi vinapendezeka mbele ya Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama mujane akiwa na watoto au wajukuu, inafaa wajifunze kwanza kutimiza mapaswa yao ya kidini kwa ajili ya jamaa zao wenyewe na kuwarudishia wazazi na babu zao mema waliyowatendea, kwa maana jambo hilo linamupendeza Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kutenda yaliyo wajib wao katika nyumba yao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Maana jambo hili ni zuri, tena lipendezalo mbele za Mungu.