1 Timothy 5:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usimtie katika orodha ya wajane mjane yeyote ambaye hajatimiza miaka sitini. Tena awe amepata kuolewa mara moja tu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mjane yeyote asiwekwe kwenye orodha ya wajane isipokuwa awe ametimiza umri wa miaka sitini, na amekuwa mke wa mume mmoja;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ili kuongezwa kwenye orodha ya wajane, mwanamke ni lazima awe na umri wa miaka 60 au zaidi, awe aliyekuwa mwaminifu kwa mume wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Usimtie katika orodha ya wajane, mjane yeyote ambaye hajatimiza miaka sitini. Tena awe amepata kuolewa mara moja tu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usimtie katika orodha ya wajane mjane yeyote ambaye hajatimiza miaka sitini. Tena awe amepata kuolewa mara moja tu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mjane ye yote asiwekwe kwenye orodha ya wajane isipokuwa awe ametimiza umri wa miaka sitini, na ambaye alikuwa mke wa mume mmoja,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mjane yeyote asiwekwe kwenye orodha ya wajane isipokuwa awe ametimiza umri wa miaka sitini, na ambaye alikuwa mke wa mume mmoja,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usimtie katika orodha ya wajane mjane yeyote ambaye hajatimiza miaka sitini. Tena awe amepata kuolewa mara moja tu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwanamke mjane apaswaye na kuandikiwa ujane ni yule aliyemaliza miaka 60, aliyekuwa mke wa mume mmoja;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usimwandike katika hesabu ya wajane mujane yeyote ambaye hajatimiza umri wa miaka makumi sita. Tena inafaa akuwe yule aliyeolewa na mume mumoja tu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mjane aandikwe, ikiwa umri wake amepata miaka sittini, isipungue, nae amekuwa mke wa mume mmoja,