1 Timothy 6:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watumwa wote wanapaswa kuwaheshimu wakuu wao ili kusiwe na sababu ya watu kulitukana jina la Mungu na mafundisho yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wote walio chini ya nira ya utumwa inawapasa kuwahesabu mabwana zao kuwa wanastahili heshima yote, ili jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wo wote walio chini ya kongwa, hali ya utumwa, na wawahesabie bwana zao kuwa wamestahili heshima yote, jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wote ambao ni watumwa waoneshe heshima kubwa kwa mabwana zao. Ndipo jina la Mungu na mafundisho yetu hayatakosolewa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watumwa wote wanapaswa kuwaheshimu wakuu wao ili kusiwe na sababu ya watu kulitukana jina la Mungu na mafundisho yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watumwa wote wanapaswa kuwaheshimu wakuu wao ili kusiwe na sababu ya watu kulitukana jina la Mungu na mafundisho yetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wote walio chini ya kongwa la utumwa inawapasa kuwahesabu mabwana zao kuwa wanastahili heshima yote, ili jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wote walio chini ya kongwa la utumwa inawapasa kuwahesabu mabwana zao kuwa wanastahili heshima yote, ili jina la Mwenyezi Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wote walio chini ya nira ya utumwa, wawachukulie bwana zao kama wanaostahili heshima yote, ili jina la Mungu na mafundisho yetu yasitukanwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watumwa wote wanapaswa kuwaheshimu wakuu wao ili kusiwe na sababu ya watu kulitukana jina la Mungu na mafundisho yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wote walio katika mafungo ya utumwa sharti wawape mabwana zao heshima zote, Jina la Mungu nao ufundisho wetu usifyozwe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wo wote walio chini ya kongwa, hali ya utumwa, na wawahesabie bwana zao kuwa wamestahili heshima yote, jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote wanaokuwa watumwa wanapaswa kuwaheshimu wabwana wao kabisa, kusudi watu wasitukane jina la Mungu na kuzarau mafundisho yetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
WO wote waiio chini ya mafungo, hali ya utumwa, wawahesabu bwana zao kuwa wamestahili heshima yote, jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.