1 Timothy 6:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye peke yake anaishi milele katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe heshima na uwezo wa milele! Amina.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
yeye pekee aishiye milele, anayedumu katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu pekee hafi, anaishi katika nuru angavu sana ambayo watu hawawezi kusogea karibu. Hakuna mtu aliyemwona Mungu; wala anayeweza kumuona. Heshima na nguvu ni zake milele. Amina.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye peke yake anaishi milele, katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe heshima na uwezo wa milele! Amina.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye peke yake anaishi milele katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe heshima na uwezo wa milele! Amina.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye peke yake hapatikani na mauti, ambaye anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yeye peke yake ambaye hapatikani na mauti, na anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyewahi kumwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye peke yake anaishi milele katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe heshima na uwezo wa milele! Amina.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni yeye peke yake asiyekufa, hukaa mwangani, msimofikiwa na mtu; hakuna mtu aliyemwona, wala hakuna awezaye kumtazama. Yeye aheshimiwe, kwa sababu nguvu ni zake kale na kale! Amin.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni yeye tu asiyeweza kufa na anayekaa katika mwangaza ambao mutu hawezi kukaribia. Hakuna mutu aliyemwona wala hakuna mutu anayeweza kumwona. Ndiye mwenye heshima na uwezo wa milele! Amina.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.