1 Timothy 6:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa namna hiyo watajiwekea hazina ambayo itakuwa kwao msingi imara kwa wakati ujao. Hapo wataweza kujipatia uhai ambao ni uhai wa kweli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa njia hii watajiwekea hazina kama msingi kwa ajili ya wakati ujao na hivyo watajipatia uzima, yaani ule uzima ambao ni wa kweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa kufanya hivi, watajiwekea hazina kwa ajili yao wenyewe. Na hazina hiyo itakuwa ni msingi imara huo utakuwa msingi imara ambao maisha yao ya siku zijazo yatajengwa. Wataweza kuwa na maisha yaliyo ya kweli kabisa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa namna hiyo watajiwekea hazina ambayo itakuwa kwao msingi imara kwa wakati ujao. Hapo wataweza kujipatia uzima ambao ni uzima wa kweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa namna hiyo watajiwekea hazina ambayo itakuwa kwao msingi imara kwa wakati ujao. Hapo wataweza kujipatia uhai ambao ni uhai wa kweli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa njia hii watajiwekea hazina kama msingi kwa ajili ya wakati ujao na hivyo watajipatia uzima, yaani, ule uzima ambao ni wa kweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa njia hii watajiwekea hazina kama msingi kwa ajili ya wakati ujao na hivyo watajipatia uzima, yaani, ule uzima ambao ni wa kweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa namna hiyo watajiwekea hazina ambayo itakuwa kwao msingi imara kwa wakati ujao. Hapo wataweza kujipatia uhai ambao ni uhai wa kweli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo ndivyo, watakavyojiwekea malimbiko yatakayokuwa msingi mzuri, siku zitakapotimia za kuupata uzima ulio wa kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa njia hii, watajiwekea akiba nzuri na yenye kudumu kwa ajili ya siku zitakazokuja kusudi wapate uzima wa kweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao illi wapate uzima wa milele.