1 Timothy 6:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Timotheo, tunza salama yote yale uliyokabidhiwa. Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ubishi wa kipumbavu juu ya kile wanachokiita watu wengine “Elimu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Timotheo, linda kile kilichowekwa amana kwako. Epuka majadiliano yasiyo ya utauwa na mabishano ambayo kwa uongo huitwa elimu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Timotheo, Mungu ameweka vitu vingi kwako uvitunze. Uvitunze vyema. Jitenge na watu wanaosema mambo yasiyofaa ambayo hayatoki kwa Mungu na wale wanaokupinga na “elimu” ambayo siyo “elimu” kabisa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Timotheo, tunza salama yote yale uliyokabidhiwa. Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ubishi wa kipumbavu juu ya kile wanachokiita watu wengine: “Elimu”.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Timotheo, tunza salama yote yale uliyokabidhiwa. Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ubishi wa kipumbavu juu ya kile wanachokiita watu wengine “Elimu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Timotheo, linda kile kilichowekwa amana kwako. Epuka majadiliano yasiyo ya utauwa na mabishano ambayo kwa uongo huitwa elimu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Timotheo, linda kile kilichowekwa amana kwako. Epuka majadiliano yasiyo ya utauwa na mabishano ambayo kwa uongo huitwa elimu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na mazungumzo yasiyo ya kimungu, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Timotheo, tunza salama yote yale uliyokabidhiwa. Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ubishi wa kipumbavu juu ya kile wanachokiita watu wengine “Elimu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Timoteo, yalinde, uliyopewa ya kuyaweka! Yakatae yale mapuzi yaliyo ya bure tu nayo yale mabishano ya utambuzi ulio wa uwongo tu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Timoteo, uchunge vizuri kile ulichopewa kwa kulinda, ukiepuka maneno ya kidunia na mabishano yasiyokuwa na maana juu ya ile watu wengine wanayoita kuwa ni elimu lakini ni uongo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Timotheo, ilinde amana, ukijiepisha na maneno yasiyo ya dini, yasiyo maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa nwongo;