1 Timothy 6:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote anayefundisha kinyume cha mambo haya, na ambaye hakubaliani na maneno ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo na mafundisho ya uchaji wa Mungu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa mtu yeyote atafundisha mafundisho mapotovu wala hakubaliani na mafundisho manyofu ya Bwana wetu Isa Al-Masihi na yale ya utauwa,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wengine wanafundisha uongo na hawakubaliani na mafundisho ya kweli ambayo yanatoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Hawakubali mafundisho ambayo yanatuongoza kumheshimu na kumpendeza Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu yeyote anayefundisha kinyume cha mambo haya, na ambaye hakubaliani na maneno ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo na mafundisho ya dini,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote anayefundisha kinyume cha mambo haya, na ambaye hakubaliani na maneno ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo na mafundisho ya uchaji wa Mungu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa mtu ye yote atafundisha mafundisho mapotovu wala hakubaliani na mafundisho manyofu ya Bwana wetu Yesu Kristo na yale ya utauwa, huyo amejivuna wala hajui kitu cho chote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa mtu yeyote atafundisha mafundisho mapotovu wala hakubaliani na mafundisho manyofu ya Bwana wetu Isa Al-Masihi na yale ya utauwa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu awaye yote akitoa mafundisho mengine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote anayefundisha kinyume cha mambo haya, na ambaye hakubaliani na maneno ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo na mafundisho ya uchaji wa Mungu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akifundisha mengine, asiposhikamana na maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo yatupayo uzima wala na ufundisho upasao wenye kumcha Mungu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mutu akifundisha mafundisho mengine, naye hakubali maneno ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo wala mafundisho yanayolingana na dini yetu,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu akifundisba mafundisho mengine, nae hayakubali maneno yenye afya va Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundislio yapatanayo na ntawa,