1 Timothy 6:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na ubishi usio na kikomo kutoka kwa watu ambao akili zao zimeharibika, na ambao hawana tena ukweli. Wanadhani dini ni njia ya kujipatia utajiri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na kuzozana kusikokoma kati ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, na ambao hudhani kwamba utauwa ni njia ya kupata faida.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Daima wanaleta shida, kwa sababu ni watu ambao kufikiri kwao kumeharibiwa. Wamepoteza ufahamu wao wa ukweli. Wanafikiri kwamba kujifanya wanamheshimu Mungu ni njia ya kupata utajiri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na ubishi usio na kikomo kutoka kwa watu ambao akili zao zimeharibika, na ambao hawana tena ukweli. Wanadhani dini ni njia ya kujipatia utajiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na ubishi usio na kikomo kutoka kwa watu ambao akili zao zimeharibika, na ambao hawana tena ukweli. Wanadhani dini ni njia ya kujipatia utajiri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na kuzozana kusikokoma kati ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli na ambao hudhani kwamba utauwa ni njia ya kupata faida.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na kuzozana kusikokoma kati ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, na ambao hudhani kwamba utauwa ni njia ya kupata faida.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kuzozana miongoni mwa watu waliopotoka katika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na ubishi usio na kikomo kutoka kwa watu ambao akili zao zimeharibika, na ambao hawana tena ukweli. Wanadhani dini ni njia ya kujipatia utajiri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
na machukivu yasiyokoma. Hao huwa kama wenye wazimu waepukao kabisa kwenye kweli, ndio wanaodhani kwamba: Kumcha Mungu ni chumo. Walio hivyo jitenge nao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na magomvi yasiyokuwa na mwisho ya watu wenye akili iliyokwisha kupotoka hata wamesahau ukweli kabisa. Ndio wale wanaozani kwamba dini ni njia ya kupata utajiri.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao,