2 Chronicles 1:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu akamjibu Solomoni, “Kwa kuwa jambo hili uliloomba limo moyoni mwako, na wala hukuomba mali, wala utajiri, wala heshima wala hukuomba wanaokuchukia waangamizwe, wala maisha marefu, lakini umeomba hekima na maarifa ili uwatawale vizuri watu wangu ambao nimekupa uwe mfalme wao,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu akamwambia Sulemani, “Kwa kuwa jambo hili ndilo shauku ya moyo wako na hukuomba mali, utajiri au heshima, wala kifo kwa ajili ya adui zako, nawe kwa kuwa hukuomba maisha marefu, bali umeomba hekima na maarifa ili kuongoza watu wangu ambao nimekufanya uwe mfalme juu yao,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu akamjibu Solomoni, “Kwa kuwa jambo hili uliloomba limo moyoni mwako, na wala hukuomba mali, wala utajiri, wala heshima wala hukuomba wanaokuchukia waangamizwe, wala maisha marefu, lakini umeomba hekima na maarifa ili uwatawale vizuri watu wangu ambao nimekupa uwe mfalme wao,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu akamwambia Solomoni, “Kwa kuwa jambo hili ndilo shauku ya moyo wako na hukuomba mali, utajiri au heshima wala kifo kwa ajili ya adui zako, nawe kwa kuwa hukuomba maisha marefu bali umeomba hekima na maarifa ili kuongoza watu wangu ambao nimekufanya uwe mfalme juu yao,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu akamwambia Sulemani, “Kwa kuwa jambo hili ndilo shauku ya moyo wako na hukuomba mali, utajiri au heshima, wala kifo kwa ajili ya adui zako, nawe kwa kuwa hukuomba maisha marefu, bali umeomba hekima na maarifa ili kuongoza watu wangu ambao nimekufanya uwe mfalme juu yao,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha ya wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwatawala watu wangu, niliokutawaza juu yao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu akamjibu Solomoni, “Kwa kuwa jambo hili uliloomba limo moyoni mwako, na wala hukuomba mali, wala utajiri, wala heshima wala hukuomba wanaokuchukia waangamizwe, wala maisha marefu, lakini umeomba hekima na maarifa ili uwatawale vizuri watu wangu ambao nimekupa uwe mfalme wao,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Mungu alipomwambia salomo: Kwa kuwa jambo kama hili limo moyoni mwako, ukaacha kuniomba mali na mapato mengi na utukufu na kufa kwa wachukivu wako, wala hukuniomba siku nyingi za kuwapo, ila umejiombea werevu wa kweli, upate kujua, jinsi utakavyowaamua walio ukoo wangu, niliokupa, uwe mfalme wao,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu akamujibu Solomono: “Kwa sababu jambo hili uliloomba liko ndani ya moyo wako, na wala haukuomba mali, wala utajiri, wala heshima wala haukuomba wanaokuchukia waangamizwe, wala maisha marefu, lakini umeomba hekima na maarifa kusudi uwatawale vizuri watu wangu ambao nimekupa ukuwe mufalme wao,