2 Chronicles 1:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Solomoni aliongeza fedha na dhahabu zikawa nyingi kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi zikapatikana kwa wingi kama mikuyu ya Shefela.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu chini ya vilima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Solomoni aliongeza fedha na dhahabu zikawa nyingi kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi zikapatikana kwa wingi kama mikuyu ya Shefela.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akaongeza fedha na dhahabu vikawa vitu vya kawaida kama vile mawe huko Yerusalemu, nayo mierezi ikawa mingi kama miti ya mikuyu chini ya vilima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Solomoni aliongeza fedha na dhahabu zikawa nyingi kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi zikapatikana kwa wingi kama mikuyu ya Shefela.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akajipatia fedha na dhahabu kuwa nyingi mle Yerusalemu kama mawe, nayo miti ya miangati akajipatia kuwa mingi kama mitamba katika nchi ya tambarare.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Solomono aliongeza feza na zahabu zikakuwa nyingi kama mawe katika Yerusalema, na mbao za mierezi zikapatikana kwa wingi kama mikuyu ya Sefela.