2 Chronicles 1:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walinunua gari moja la farasi kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150 za fedha. Kisha waliwauzia wafalme wa Wahiti na Shamu farasi hao na magari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliagiza magari ya vita kutoka Misri kwa bei ya shekeli mia sita za fedha, na farasi kwa shekeli mia moja na hamsini. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao hupandisha, na kuleta kutoka Misri gari kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi kwa mia na hamsini, vivyo watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walinunua gari moja la farasi kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150 za fedha. Kisha waliwauzia wafalme wa Wahiti na Shamu farasi hao na magari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walileta magari ya vita kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha kwa kila moja, na kwa kila farasi shekeli 150. Pia wakawapeleka ili kuwauzia wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waliagiza magari kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha, na farasi kwa shekeli 150. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walipandisha na kununua gari kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha; na farasi kwa mia moja na hamsini, vivyo hivyo wakawauzia wafalme wote Wahiti na wafalme wa Shamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walinunua gari moja la farasi kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150 za fedha. Kisha waliwauzia wafalme wa Wahiti na Shamu farasi hao na magari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Magari, waliyoyatoa Misri na kuyapeleka kwao, moja lilikuwa fedha 600, na farasi mmoja fedha 150.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao hupandisha, na kuleta kutoka Misri gari kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi kwa mia na hamsini, vivyo watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walinunua gari moja la vita kutoka Misri kwa bei ya vikoroti mia sita za feza, na farasi mumoja kwa vikoroti mia moja na makumi tano za feza. Kisha waliwauzishia wafalme wa Wahiti na wa Wasuria farasi hao na magari.