2 Chronicles 1:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akaandamana nao hadi mahali pa ibada huko Gibeoni. Walikwenda huko kwa sababu hapo ndipo mahali lilipokuwa hema la mkutano la Mungu alilolitengeneza Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, nyikani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Sulemani na kusanyiko lote wakakwea hadi mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni. Hema la Kukutania la Mungu, ambalo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alikuwa amelitengeneza huko jangwani, lilikuwa Gibeoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Sulemani akaenda mahali pa juu pa Gibeoni, na kusanyiko lote naye; kwani ndipo ilipokuwako hema ya kukutania ya Mungu, aliyoifanya Musa mtumishi wa Bwana jangwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akaandamana nao hadi mahali pa ibada huko Gibeoni. Walikwenda huko kwa sababu hapo ndipo mahali lilipokuwa hema la mkutano la Mungu alilolitengeneza Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, nyikani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Solomoni na kusanyiko lote wakakwea mpaka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kwa kuwa huko ndiko hema la Mungu la Mkutano lilipokuwa, ambalo Mose mtumishi wa BWANA alikuwa amelitengeneza huko jangwani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Sulemani na kusanyiko lote wakakwea mpaka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kwa kuwa huko ndiko Hema la Kukutania la Mungu lilipokuwa, ambalo Musa mtumishi wa bwana alikuwa amelitengeneza huko jangwani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Sulemani akaenda mahali pa juu pa Gibeoni, na kusanyiko lote naye; kwani ndipo lilipokuwako hema la kukutania la Mungu, alilolifanya Musa mtumishi wa BWANA jangwani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akaandamana nao hadi mahali pa ibada huko Gibeoni. Walikwenda huko kwa sababu hapo ndipo mahali lilipokuwa hema la mkutano la Mungu alilolitengeneza Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, nyikani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakaenda, yeye Salomo pamoja na huo mkutano wote, kilimani kwa Gibeoni, kwani ndiko, lilikokuwa Hema la Mkutano la Mungu, Mose, mtumishi wa Bwana, alilolitengeneza nyikani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Sulemani akaenda mahali pa juu pa Gibeoni, na kusanyiko lote naye; kwani ndipo ilipokuwako hema ya kukutania ya Mungu, aliyoifanya Musa mtumishi wa BWANA jangwani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akaandamana nao mpaka pahali pa ibada kule Gibeoni. Walikwenda kule kwa sababu pale ndipo pahali palipokuwa hema la mukutano la Mungu ambalo Musa mutumishi wa Yawe, alilotengeneza katika jangwa.