2 Chronicles 1:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, madhabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli, mwana wa Uri na mjukuu wa Huri, pia ilikuwa huko Gibeoni mbele ya hema takatifu la Mwenyezi-Mungu. Hapo mfalme Solomoni na watu wote wakamwomba Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yale madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza yalikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya Mwenyezi Mungu, hivyo Sulemani na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena madhabahu ya shaba, aliyoifanyiza Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwako huko mbele ya maskani ya Bwana; Sulemani na kusanyiko wakaiendea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, madhabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli, mwana wa Uri na mjukuu wa Huri, pia ilikuwa huko Gibeoni mbele ya hema takatifu la Mwenyezi-Mungu. Hapo mfalme Solomoni na watu wote wakamwomba Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ile madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza ilikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya BWANA Mungu, hivyo Solomoni na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yale madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza yalikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya bwana Mwenyezi Mungu, hivyo Sulemani na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena madhabahu ya shaba, aliyoifanya Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwako huko mbele ya maskani ya BWANA; Sulemani na kusanyiko wakaiendea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, madhabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli, mwana wa Uri na mjukuu wa Huri, pia ilikuwa huko Gibeoni mbele ya hema takatifu la Mwenyezi-Mungu. Hapo mfalme Solomoni na watu wote wakamwomba Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini meza ya shaba ya kutambikia, aliyoitengeneza Besaleli, mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwa huko mbele ya Kao lake Bwana; ndiyo, Salomo na mkutano waliyoiendea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena madhabahu ya shaba, aliyoifanyiza Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwako huko mbele ya maskani ya BWANA; Sulemani na kusanyiko wakaiendea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, mazabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli, mwana wa Uri na mujukuu wa Huri, ilikuwa kule Gibeoni mbele ya hema takatifu la Yawe. Hapo mufalme Solomono na watu wote wakamwomba Yawe.