2 Chronicles 1:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni alipanda mbele ya madhabahu ya shaba iliyokuwa kwenye hema la mkutano. Hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu, akatoa tambiko 1,000 za kuteketezwa juu ya madhabahu hayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani akapanda huko yalikokuwa madhabahu ya shaba mbele za Mwenyezi Mungu katika Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu elfu moja za sadaka za kuteketezwa juu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za Bwana, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni alipanda mbele ya madhabahu ya shaba iliyokuwa kwenye hema la mkutano. Hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu, akatoa tambiko 1,000 za kuteketezwa juu ya madhabahu hayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Solomoni akapanda huko ilikokuwa madhabahu ya shaba mbele za BWANA katika Hema la Kukutania na kutoa dhabihu 1,000 za sadaka za kuteketezwa juu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sulemani akapanda huko yalikokuwa madhabahu ya shaba mbele za bwana katika Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu 1,000 za sadaka za kuteketezwa juu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za BWANA, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni alipanda mbele ya madhabahu ya shaba iliyokuwa kwenye hema la mkutano. Hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu, akatoa tambiko 1,000 za kuteketezwa juu ya madhabahu hayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo akamtambikia Bwana huko juu ya ile meza ya shaba iliyokuwa penye Hema la Mkutano, akatoa ng'ombe elfu za tambiko za kuteketezwa nzima juu yake hiyo meza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za BWANA, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono akapanda mbele ya mazabahu ya shaba iliyokuwa kwenye hema la mukutano. Pale mbele ya Yawe, akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya mazabahu yale.