2 Chronicles 1:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, ee Mungu, Mwenyezi-Mungu, itimize ahadi uliyompa baba yangu Daudi. Umenitawaza niwe mfalme juu ya watu hawa walio wengi kama mavumbi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa, Bwana Mwenyezi Mungu, ahadi yako kwa baba yangu Daudi na ithibitike, kwa kuwa umenifanya mimi mfalme juu ya watu ambao ni wengi kama mavumbi ya nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa, Ee Bwana Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, ee Mungu, Mwenyezi-Mungu, itimize ahadi uliyompa baba yangu Daudi. Umenitawaza niwe mfalme juu ya watu hawa walio wengi kama mavumbi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa, BWANA Mungu, ahadi yako kwa baba yangu Daudi na ithibitike, kwa kuwa umenifanya mimi mfalme juu ya watu ambao ni wengi kama mavumbi ya nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa, bwana Mwenyezi Mungu, ahadi yako kwa baba yangu Daudi na ithibitike, kwa kuwa umenifanya mimi mfalme juu ya watu ambao ni wengi kama mavumbi ya nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, ee Mungu, Mwenyezi-Mungu, itimize ahadi uliyompa baba yangu Daudi. Umenitawaza niwe mfalme juu ya watu hawa walio wengi kama mavumbi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa Bwana Mungu, neno lako, ulilomwambia baba yangu Dawidi, na litiwe nguvu, litimie! Kwani wewe umenipa kuwa mfalme wa watu walio wengi kama mavumbi ya nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, ee Mungu, Yawe, utimize ahadi uliyomupa Daudi baba yangu. Umeniweka kuwa mufalme juu ya watu hawa wanaokuwa wengi kama mavumbi.