2 Chronicles 10:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watu wote wa Israeli walipoona kwamba mfalme hakuwajali walimwambia, “Tuna sehemu gani kwa Daudi? Hatuna urithi katika mwana wa Yese. Kila mmoja na arudi nyumbani kwake, enyi watu wa Israeli. Itunze nyumba yako mwenyewe, ee Daudi.” Hivyo watu wote wa Israeli wakarudi makwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: “Je, tuna fungu gani kwa Daudi? Tuna urithi gani kwa mwana wa Yese? Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli, angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hawasikilizi, watu wakamjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli, kila mtu; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Daudi. Basi wakaenda zao Israeli wote hemani kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watu wote wa Israeli walipoona kwamba mfalme hakuwajali walimwambia, “Tuna sehemu gani kwa Daudi? Hatuna urithi katika mwana wa Yese. Kila mmoja na arudi nyumbani kwake, enyi watu wa Israeli. Itunze nyumba yako mwenyewe, ee Daudi.” Hivyo watu wote wa Israeli wakarudi makwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: “Tuna fungu gani kwa Daudi? Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese. Nendeni kwenye mahema yenu, Ee Israeli, angalia nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: “Tuna fungu gani kwa Daudi? Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese. Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli, angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hawasikilizi, watu wakamjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; kila mtu aende zake hemani, enyi Israeli, sasa itunze nyumba yako mwenyewe ewe Daudi. Basi wakaenda zao Israeli wote hemani kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watu wote wa Israeli walipoona kwamba mfalme hakuwajali walimwambia, “Tuna sehemu gani kwa Daudi? Hatuna urithi katika mwana wa Yese. Kila mmoja na arudi nyumbani kwake, enyi watu wa Israeli. Itunze nyumba yako mwenyewe, ee Daudi.” Hivyo watu wote wa Israeli wakarudi makwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waisiraeli wote walipoona, ya kuwa mfalme hakuwasikia, ndipo, watu walipomjibu mfalme kwamba: Sisi tuna bia gani na Dawidi? Hatuna fungu lo lote kwake mwana wa Isai. Waisiraeli, haya! Rudini sasa mahemani kwenu, kila mtu kwake! Nawe Dawidi, na uuangalie mwenyewe mlango wako! Ndipo, Waisiraeli wote walipokwenda mahemani kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hawasikilizi, watu wakamjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli, kila mtu; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Daudi. Basi wakaenda zao Israeli wote hemani kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini watu wote wa Israeli walipoona kwamba mufalme hakuwajali walimwambia: “Hatuna ushirika na Daudi! Hatuna urizi kutoka kwa mwana wa Yese. Kila mumoja arudie kwake, enyi watu wa Israeli! Utunze nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wote wakarudi kila mutu kwake.