2 Chronicles 11:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walawi waliyaacha malisho yao, na maeneo yao mengine kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwakataza kumtumikia Mwenyezi-Mungu kama makuhani wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia Walawi wakaacha maeneo yao ya malisho na mali yao, wakaja Yuda na Yerusalemu kwa sababu Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewakataa wasiwe makuhani wa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwani Walawi wakaacha malisho yao, na milki yao, wakaja Yuda na Yerusalemu; kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwatupa, ili wasimfanyie Bwana ukuhani;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walawi waliyaacha malisho yao, na maeneo yao mengine kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwakataza kumtumikia Mwenyezi-Mungu kama makuhani wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia Walawi wakaacha maeneo yao ya malisho na mali zao, wakaja Yuda na Yerusalemu kwa sababu Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewakataa wasiwe makuhani wa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia Walawi wakaacha maeneo yao ya malisho na mali zao, wakaja Yuda na Yerusalemu kwa sababu Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewakataa wasiwe makuhani wa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walawi wakaacha malisho yao, na milki yao, wakaja Yuda na Yerusalemu; kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwakataza, ili wasimfanyie BWANA ukuhani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walawi waliyaacha malisho yao, na maeneo yao mengine kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwakataza kumtumikia Mwenyezi-Mungu kama makuhani wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Walawi wakayaacha malisho na mapato yao, wakaenda Uyuda na Yerusalemu, kwa kuwa Yeroboamu na wanawe waliwatupa, waiswe watambikaji wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwani Walawi wakaacha malisho yao, na milki yao, wakaja Yuda na Yerusalemu; kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwatupa, ili wasimfanyie BWANA ukuhani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walawi wakaacha mashamba yao ya malisho ya nyama, na maeneo yao mengine kwa sababu Yeroboamu na wana wake waliwakataza kumutumikia Yawe kama vile makuhani wa Yawe.