2 Chronicles 11:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote ambao walikuwa wamenuia kwa moyo wa dhati kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kutoka katika makabila yote ya Israeli, waliandamana na Walawi hadi Yerusalemu ili wapate kumtolea tambiko Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtolea Mwenyezi Mungu dhabihu, Mungu wa baba zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta Bwana, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu Bwana, Mungu wa baba zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote ambao walikuwa wamenuia kwa moyo wa dhati kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kutoka katika makabila yote ya Israeli, waliandamana na Walawi hadi Yerusalemu ili wapate kumtolea tambiko Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtolea BWANA dhabihu, Mungu wa baba zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafuta bwana, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtolea bwana dhabihu, Mungu wa baba zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote ambao walikuwa wamenuia kwa moyo wa dhati kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kutoka katika makabila yote ya Israeli, waliandamana na Walawi hadi Yerusalemu ili wapate kumtolea tambiko Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mashina yote ya Isiraeli watu waliojipa mioyo ya kumtafuta Bwana Mungu wa Isiraeli wakawafuata wale, wakaja Yerusalemu kumtolea Bwana Mungu wa baba zao ng'ombe za tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote ambao walikuwa wamekusudia kwa moyo kumwabudu Yawe, Mungu wa Israeli, kutoka katika makabila yote ya Israeli, waliandamana na Walawi mpaka Yerusalema kusudi wapate kumutolea sadaka Yawe, Mungu wa babu zao.