2 Chronicles 11:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mimi Bwana nasema, ‘Msiende wala msipigane na ndugu zenu. Rudini kila mtu nyumbani kwake, maana hayo yaliyotokea ni kama nilivyopanga.’” Basi wakatii ujumbe wa Mwenyezi-Mungu, wakarudi nyumbani, wala hawakwenda kupigana na Yeroboamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la Mwenyezi Mungu na kurudi, wakaacha kwenda kupigana dhidi ya Yeroboamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakayasikiliza maneno ya Bwana, wakarudi katika kumwendea Yeroboamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mimi Bwana nasema, ‘Msiende wala msipigane na ndugu zenu. Rudini kila mtu nyumbani kwake, maana hayo yaliyotokea ni kama nilivyopanga.’” Basi wakatii ujumbe wa Mwenyezi-Mungu, wakarudi nyumbani, wala hawakwenda kupigana na Yeroboamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hili ndilo asemalo BWANA, ‘Usipande kwenda kupigana dhidi ya ndugu zako Waisraeli. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la BWANA na kurudi nyumbani, wakaacha kwenda kupigana dhidi ya Yeroboamu kama BWANA alivyokuwa ameagiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Hili ndilo asemalo bwana: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la bwana na wakaacha kwenda kupigana dhidi ya Yeroboamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi wakayatii maneno ya BWANA wakarudi wasiende kupigana na Yeroboamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mimi Bwana nasema, ‘Msiende wala msipigane na ndugu zenu. Rudini kila mtu nyumbani kwake, maana hayo yaliyotokea ni kama nilivyopanga.’” Basi wakatii ujumbe wa Mwenyezi-Mungu, wakarudi nyumbani, wala hawakwenda kupigana na Yeroboamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Msipande kwenda kupigana na ndugu zenu! Rudini kila mtu nyumbani kwake! Kwani jambo hili limefanywa na mimi. Walipoyasikia maneno haya ya Bwana wakarudi wakiacha kumwendea Yeroboamu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakayasikiliza maneno ya BWANA, wakarudi katika kumwendea Yeroboamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana anasema hivi: ‘Musiende wala musipigane na wandugu zenu. Murudie kila mutu kwake, maana yale yaliyotokea ni kwa kufuata mupango wangu.’ ” Basi wakatii ujumbe wa Yawe, wakarudia kila mutu kwake, wala hawakwenda kupigana na Yeroboamu.