2 Chronicles 12:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Matendo yote ya mfalme Rehoboamu ya mwanzo mpaka ya mwisho na rekodi ya ukoo yameandikwa katika kitabu cha Kumbukumbu za nabii Shemaya, na Kumbukumbu za Ido Mwonaji. Wakati huu wote, kulikuwa na vita vya mfululizo kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwa na vita vya mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Matendo yote ya mfalme Rehoboamu ya mwanzo mpaka ya mwisho na rekodi ya ukoo yameandikwa katika kitabu cha Kumbukumbu za nabii Shemaya, na Kumbukumbu za Ido Mwonaji. Wakati huu wote, kulikuwa na vita vya mfululizo kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, tangu mwanzo mpaka mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwako na vita mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, tangu mwanzo mpaka mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwako na vita mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza hadi ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Matendo yote ya mfalme Rehoboamu ya mwanzo mpaka ya mwisho na rekodi ya ukoo yameandikwa katika kitabu cha Kumbukumbu za nabii Shemaya, na Kumbukumbu za Ido Mwonaji. Wakati huu wote, kulikuwa na vita vya mfululizo kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mambo ya Rehabeamu, ya kwanza na ya mwisho, hayakuandikwa kwenye mambo ya mfumbuaji Semaya na ya mchunguzaji Ido, kama mambo ya wakale yalivyoandikwa? Lakini Rehabeamu na Yeroboamu walikuwa wakipigana vita siku zile zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Matendo ya mufalme Rehoboamu tangu mwanzo mpaka ya mwisho yameandikwa katika kitabu cha “Mambo ya Siku ya nabii Semaya”, na “Mambo ya Siku ya nabii Ido.” Wakati huu wote, kulikuwa vita ya mufululizo kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.