2 Chronicles 12:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mfalme Shishaki wa Misri aliushambulia Yerusalemu, akaichukua hazina yote ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na ya ikulu, pamoja na ngao za dhahabu alizozitengeneza mfalme Solomoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shishaki mfalme wa Misri alipoishambulia Yerusalemu, alichukua hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa amezitengeneza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Shishaki, mfalme wa Misri, akapanda juu ya Yerusalemu, akazichukua hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao za dhahabu alizozifanya Sulemani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mfalme Shishaki wa Misri aliushambulia Yerusalemu, akaichukua hazina yote ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na ya ikulu, pamoja na ngao za dhahabu alizozitengeneza mfalme Solomoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shishaki mfalme wa Misri alipoishambulia Yerusalemu, alichukua hazina za Hekalu la BWANA na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao za dhahabu ambazo Solomoni alikuwa amezitengeneza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shishaki mfalme wa Misri alipoishambulia Yerusalemu, alichukua hazina za Hekalu la bwana na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa amezitengeneza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Shishaki, mfalme wa Misri, akaushambulia Yerusalemu, akazichukua hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao za dhahabu alizozitengeneza Sulemani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mfalme Shishaki wa Misri aliushambulia Yerusalemu, akaichukua hazina yote ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na ya ikulu, pamoja na ngao za dhahabu alizozitengeneza mfalme Solomoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sisaki, mfalme wa Misri, akapanda, akaujia Yerusalemu, akavichukua vilimbiko vya Nyumbani mwa Bwana navyo vilimbiko vya nyumbani mwa mfalme, vyote pia akavichukua, nazo ngao za dhahabu, Salomo alizozitengeneza, akazichukua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Shishaki, mfalme wa Misri, akapanda juu ya Yerusalemu, akazichukua hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao za dhahabu alizozifanya Sulemani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mufalme Sisaki wa Misri akashambulia muji Yerusalema, akaichukua hazina yote ya nyumba ya Yawe na ya nyumba ya kifalme, pamoja na ngao za zahabu ambazo mufalme Solomono alizozitengeneza.