2 Chronicles 13:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila siku asubuhi na jioni, makuhani humtolea sadaka za kuteketezwa nzima, na kumfukizia ubani wenye harufu nzuri, tena hupanga juu ya meza ya dhahabu safi, mikate ya kuwekwa mbele ya Mungu, na kukitunza kinara cha dhahabu na kuziwasha taa kila siku jioni. Sisi tunayafuata maagizo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, lakini nyinyi mmemwacha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila asubuhi na jioni wao hutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwa Mwenyezi Mungu. Wao huweka mikate juu ya meza takatifu, na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Sisi tunazishika kanuni za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nao humtolea Bwana kila asubuhi, na kila jioni, sadaka za kuteketezwa na fukizo la manukato; mikate ya wonyesho pia huiweka kwa taratibu yake juu ya meza takatifu, na kinara cha dhahabu chenye taa zake, kuwaka kila jioni; kwa maana sisi twayalinda malinzi ya Bwana, Mungu wetu; bali ninyi mmemwacha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila siku asubuhi na jioni, makuhani humtolea sadaka za kuteketezwa nzima, na kumfukizia ubani wenye harufu nzuri, tena hupanga juu ya meza ya dhahabu safi, mikate ya kuwekwa mbele ya Mungu, na kukitunza kinara cha dhahabu na kuziwasha taa kila siku jioni. Sisi tunayafuata maagizo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, lakini nyinyi mmemwacha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makuhani wanaomtumikia BWANA ni wana wa Aroni nao Walawi wakiwasaidia kila asubuhi na jioni kutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwa BWANA. Huweka mikate juu ya meza safi kwa taratibu za kiibada na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Tunazishika kanuni za BWANA Mungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila asubuhi na jioni wao hutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwa bwana. Wao huweka mikate juu ya meza safi kwa taratibu za kiibada na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Sisi tunazishika kanuni za bwana Mwenyezi Mungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nao humtolea BWANA kila asubuhi, na kila jioni, sadaka za kuteketezwa na fukizo la manukato; mikate ya wonyesho pia huiweka kwa taratibu yake juu ya meza takatifu, na kinara cha dhahabu chenye taa zake, kuwaka kila jioni; kwa maana sisi tunayatunza maagizo ya BWANA, Mungu wetu; bali ninyi mmemwacha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila siku asubuhi na jioni, makuhani humtolea sadaka za kuteketezwa nzima, na kumfukizia ubani wenye harufu nzuri, tena hupanga juu ya meza ya dhahabu safi, mikate ya kuwekwa mbele ya Mungu, na kukitunza kinara cha dhahabu na kuziwasha taa kila siku jioni. Sisi tunayafuata maagizo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, lakini nyinyi mmemwacha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kila kunapokucha na kila kunapokuchwa humvukizia Bwana wakimteketezea ng'ombe za tambiko na kumvikizia mavukizo yanukayo vizuri, tena humwekea mikate katika meza iliyo ya dhahabu tupu, tena hukiwasha kinara cha dhahabu na taa zake kila kunapokuchwa, kwani sisi tunaushika ulinzi wa Bwana Mungu wetu, lakini ninyi mmemwacha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nao humtolea BWANA kila asubuhi, na kila jioni, sadaka za kuteketezwa na fukizo la manukato; mikate ya wonyesho pia huiweka kwa taratibu yake juu ya meza takatifu, na kinara cha dhahabu chenye taa zake, kuwaka kila jioni; kwa maana sisi twayalinda malinzi ya BWANA, Mungu wetu; bali ninyi mmemwacha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila siku asubui na magaribi, makuhani wanamutolea sadaka za kuteketezwa na kumufukizia ubani wenye harufu nzuri, tena wanapanga mikate inayotolewa na Mungu juu ya meza ya zahabu safi, na kutunza kinara cha zahabu na kuwasha taa kila siku magaribi. Sisi tunayafuata maagizo ya Yawe, Mungu wetu, lakini ninyi mumemwacha.