2 Chronicles 13:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hebu tazameni, Mungu mwenyewe ndiye kiongozi wetu na makuhani wake wanazo tarumbeta zao tayari kuzipiga ili kutupa ishara ya kuanza vita dhidi yenu. Enyi watu wa Israeli, acheni kupigana vita dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu. Hamwezi kushinda!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu yu pamoja nasi; yeye ndiye kiongozi wetu. Makuhani wake wakiwa na tarumbeta zao watapiga baragumu ya vita dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, kwa maana hamtashinda.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, Mungu yu pamoja nasi atutangulie, na makuhani wake wenye mapanda, ili wapige sauti ya kugutusha juu yenu. Enyi wana wa Israeli, msipigane na Bwana, Mungu wa baba zenu; kwani hamtafanikiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hebu tazameni, Mungu mwenyewe ndiye kiongozi wetu na makuhani wake wanazo tarumbeta zao tayari kuzipiga ili kutupa ishara ya kuanza vita dhidi yenu. Enyi watu wa Israeli, acheni kupigana vita dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu. Hamwezi kushinda!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu yu pamoja nasi, yeye ndiye kiongozi wetu. Makuhani wake wakiwa na tarumbeta zao watapiga baragumu ya vita dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane dhidi ya BWANA, Mungu wa baba zenu, kwa maana hamtashinda.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu yu pamoja nasi, yeye ndiye kiongozi wetu. Makuhani wake wakiwa na tarumbeta zao watapiga baragumu ya vita dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane dhidi ya bwana, Mungu wa baba zenu, kwa maana hamtashinda.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, Mungu yu pamoja nasi atutangulie, na makuhani wake wenye parapanda, ili wapige sauti ya kuanza vita juu yenu. Enyi wana wa Israeli, msipigane na BWANA, Mungu wa baba zenu; kwani hamtafanikiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hebu tazameni, Mungu mwenyewe ndiye kiongozi wetu na makuhani wake wanazo tarumbeta zao tayari kuzipiga ili kutupa ishara ya kuanza vita dhidi yenu. Enyi watu wa Israeli, acheni kupigana vita dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu. Hamwezi kushinda!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na mwone, ya kuwa Mungu yuko kwetu, ndiye anayetutangulia, nao watambikaji wake watapiga matarumbeta ya kuvumisha sana, wawazomee ninyi! Wana wa Isiraeli, msije kupigana na Mungu wa baba zenu! Kwani hamtafanikiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, Mungu yu pamoja nasi atutangulie, na makuhani wake wenye mapanda, ili wapige sauti ya kugutusha juu yenu. Enyi wana wa Israeli, msipigane na BWANA, Mungu wa baba zenu; kwani hamtafanikiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na muangalie, Mungu mwenyewe ndiye kiongozi wetu na makuhani wake wako na baragumu zao tayari kuzipiga kwa kupana kitambulisho cha kuanza vita juu yenu. Enyi watu wa Israeli, muache kupigana vita na Yawe, Mungu wa babu zenu. Hamuwezi kushinda!”