2 Chronicles 13:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Abiya aliendelea kupata nguvu zaidi. Akaoa wanawake kumi na wanne, akapata watoto wa kiume ishirini na wawili na mabinti kumi na sita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Abiya akapata nguvu. Alioa wanawake kumi na wanne na alikuwa na wana ishirini na wawili na binti kumi na sita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ila Abiya akapata nguvu, akaoa wake kumi na wanne, akazaa wana ishirini na wawili, na binti kumi na sita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Abiya aliendelea kupata nguvu zaidi. Akaoa wanawake kumi na wanne, akapata watoto wa kiume ishirini na wawili na mabinti kumi na sita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Abiya akapata nguvu. Alioa wanawake kumi na wanne na alikuwa na wana ishirini na wawili na binti kumi na sita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Abiya akapata nguvu. Alioa wanawake kumi na wanne na alikuwa na wana ishirini na wawili na binti kumi na sita.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ila Abiya akapata nguvu, akaoa wake kumi na wanne, akazaa watoto wa kiume ishirini na wawili, na mabinti kumi na sita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Abiya aliendelea kupata nguvu zaidi. Akaoa wanawake kumi na wanne, akapata watoto wa kiume ishirini na wawili na mabinti kumi na sita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Abia akajipatia nguvu, akajichukulia wanawake 18, akazaa wana wa kiume 22 na wa kike 16.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ila Abiya akapata nguvu, akaoa wake kumi na wanne, akazaa wana ishirini na wawili, na binti kumi na sita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Abiya aliendelea kupata nguvu zaidi. Akaoa wanawake kumi na wane, akazaa wana makumi mbili na wawili na wabinti kumi na sita.