2 Chronicles 13:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abiya alijiandaa kupigana vita akiwa na jeshi la askari hodari 400,000, naye Yeroboamu akamkabili na jeshi lake la askari hodari 800,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Abiya aliingia vitani na jeshi la watu elfu mia nne wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu elfu mia nane wenye uwezo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Abiya akapanga vita mwenye jeshi la watu hodari wa vita, watu wateule mia nne elfu; naye Yeroboamu akapanga vita juu yake mwenye watu wateule mia nane elfu, waliokuwa waume mashujaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abiya alijiandaa kupigana vita akiwa na jeshi la askari hodari 400,000, naye Yeroboamu akamkabili na jeshi lake la askari hodari 800,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Abiya aliingia vitani na jeshi la watu 400,000 wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu 800,000 wenye uwezo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Abiya aliingia vitani na jeshi la watu 400,000 wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu 800,000 wenye uwezo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Abiya akapanga vita akiwa na jeshi la watu hodari wa vita, watu wateule elfu mia nne; naye Yeroboamu akapanga vita juu yake akiwa na watu wateule elfu mia nane, waliokuwa wanaume mashujaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abiya alijiandaa kupigana vita akiwa na jeshi la askari hodari 400,000, naye Yeroboamu akamkabili na jeshi lake la askari hodari 800,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Abia akajifunga kwenda vitani mwenye vikosi vya mafundi wa vita, watu 400000 waliochaguliwa. Naye Yeroboamu akajipanga vitani mwenye watu 800000 waliochaguliwa kwa kuwa mafundi wa vita wenye nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Abiya akapanga vita mwenye jeshi la watu hodari wa vita, watu wateule mia nne elfu; naye Yeroboamu akapanga vita juu yake mwenye watu wateule mia nane elfu, waliokuwa waume mashujaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abiya alijitayarisha kupigana vita akiwa na jeshi la waaskari hodari elfu mia ine, naye Yeroboamu akajitayarisha na jeshi lake la waaskari hodari elfu mia nane.