2 Chronicles 13:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, hamkuwafukuza makuhani wa Mwenyezi-Mungu, wana wa Aroni, kadhalika na Walawi, na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama wafanyavyo watu wa mataifa mengine? Yeyote ajaye kwenu kujiweka wakfu na ndama dume ama kondoo madume saba, huwa kuhani wa vitu ambavyo si miungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini je, hamkuwafukuza makuhani wa Mwenyezi Mungu, wana wa Haruni na Walawi na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama yafanyavyo mataifa ya nchi nyingine? Yeyote anayekuja kujiweka wakfu akiwa na ndama dume na kondoo dume saba aweza kuwa kuhani wa kile ambacho ni miungu kwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Hamkuwafukuza makuhani wa Bwana, wana wa Haruni, na Walawi; mkajifanyia makuhani kama wafanyavyo watu wa nchi nyingine? Hata ye yote ajaye kujifanya wakfu na ndama, na kondoo waume saba, aweza kuwa kuhani wa hiyo isiyo miungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, hamkuwafukuza makuhani wa Mwenyezi-Mungu, wana wa Aroni, kadhalika na Walawi, na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama wafanyavyo watu wa mataifa mengine? Yeyote ajaye kwenu kujiweka wakfu na ndama dume ama kondoo madume saba, huwa kuhani wa vitu ambavyo si miungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini je, hamkuwafukuza makuhani wa BWANA, wana wa Aroni na Walawi na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama yafanyavyo mataifa ya nchi nyingine? Ye yote anayekuja kujiweka wakfu akiwa na ndama dume na kondoo waume saba aweza kuwa kuhani wa kile ambacho ni miungu kwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini je, hamkuwafukuza makuhani wa bwana, wana wa Haruni na Walawi na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama yafanyavyo mataifa ya nchi nyingine? Yeyote anayekuja kujiweka wakfu akiwa na ndama dume na kondoo dume saba aweza kuwa kuhani wa kile ambacho ni miungu kwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Hamkuwafukuza makuhani wa BWANA, wana wa Haruni, na Walawi; mkajifanyia makuhani kama wafanyavyo watu wa nchi nyingine? Hata yeyote ajaye kujifanya wakfu na ndama, na kondoo dume saba, aweza kuwa kuhani wa hiyo isiyo miungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, hamkuwafukuza makuhani wa Mwenyezi-Mungu, wana wa Aroni, kadhalika na Walawi, na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama wafanyavyo watu wa mataifa mengine? Yeyote ajaye kwenu kujiweka wakfu na ndama dume ama kondoo madume saba, huwa kuhani wa vitu ambavyo si miungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hamkuwafukuza watambikaji wa Bwana, wana wa Haroni, pamoja na Walawi, mkajifanyizia watambikaji, kama makabila ya nchi hizi? Kila ajaye na kuleta mtoto mume wa ng'ombe na madume saba ya kondoo, apate kulijaza gao lake, basi, hupata kuwa mtambikaji wao isiyo miungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Hamkuwafukuza makuhani wa BWANA, wana wa Haruni, na Walawi; mkajifanyia makuhani kama wafanyavyo watu wa nchi nyingine? Hata ye yote ajaye kujifanya wakfu na ndama, na kondoo waume saba, aweza kuwa kuhani wa hiyo isiyo miungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hamukuwafukuza makuhani wa Yawe, wana wa Haruni, vilevile na Walawi, na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama vile watu wa mataifa mengine wanavyofanya? Yeyote anayekuja kwenu kujitakasa na mwana-ngombe dume au kondoo dume anakuwa kuhani wa vitu ambavyo si miungu.