2 Chronicles 14:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asa pamoja na wanajeshi wake wakawafuatilia mpaka Gerari, wakawaua Waethiopia wengi sana, asibaki hata mmoja, kwani walikuwa wamekwisha shindwa na Mwenyezi-Mungu pamoja na jeshi lake. Jeshi la Yuda lilichukua nyara nyingi sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye Asa na jeshi lake wakawafuatia hadi Gerari. Idadi kubwa ya Wakushi ilianguka hata wasiweze kuinuka tena, wakapondapondwa mbele za Mwenyezi Mungu na majeshi yake. Watu wa Yuda wakachukua nyara nyingi sana;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Asa na watu waliokuwa pamoja naye wakawafuata mpaka Gerari; nao wengi wakaanguka wa Wakushi hata wasiweze kupona; kwa sababu waliangamizwa mbele za Bwana, na mbele ya jeshi lake; na hao wakachukua mateka mengi sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asa pamoja na wanajeshi wake wakawafuatilia mpaka Gerari, wakawaua Waethiopia wengi sana, asibaki hata mmoja, kwani walikuwa wamekwisha shindwa na Mwenyezi-Mungu pamoja na jeshi lake. Jeshi la Yuda lilichukua nyara nyingi sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye Asa na jeshi lake wakawafuatia mpaka Gerari. Idadi kubwa ya Wakushi ilianguka hata wasiweze kuinuka tena, wakapondwapondwa mbele za BWANA na majeshi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye Asa na jeshi lake wakawafuatia mpaka Gerari. Idadi kubwa ya Wakushi ilianguka hata wasiweze kuinuka tena, wakapondapondwa mbele za bwana na majeshi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Asa na watu waliokuwa pamoja naye wakawafuata mpaka Gerari; wakawaua Wakushi wengi sana asipone hata mmoja; kwa sababu waliangamizwa mbele za BWANA, na mbele ya jeshi lake; na hao wakachukua mateka wengi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asa pamoja na wanajeshi wake wakawafuatilia mpaka Gerari, wakawaua Waethiopia wengi sana, asibaki hata mmoja, kwani walikuwa wamekwisha shindwa na Mwenyezi-Mungu pamoja na jeshi lake. Jeshi la Yuda lilichukua nyara nyingi sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asa akawakimbiza pamoja na hao watu, aliokuwa nao, mpaka Gerari; kwa Wanubi watu wakauawa kabisa, hakusalia kwao waliopona, kwani walivunjwa mbele ya Bwana na mbele ya vikosi vyake. Kisha Wayuda wakachukua mateka mengi sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Asa na watu waliokuwa pamoja naye wakawafuata mpaka Gerari; nao wengi wakaanguka wa Wakushi hata wasiweze kupona; kwa sababu waliangamizwa mbele za BWANA, na mbele ya jeshi lake; na hao wakachukua mateka mengi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Likaharibu miji yote iliyokuwa kandokando ya Gerari, kwa kuwa watu waliokuwa katika miji ile, walipatwa na hofu ya Yawe. Likabeba mali nyingi kutoka katika miji ile, kwa sababu kulikuwa mali mengi sana.