2 Chronicles 14:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akawaambia watu wa Yuda, “Na tuiimarishe miji kwa kuizungushia kuta na minara na malango yenye makomeo. Nchi bado imo mikononi mwetu kwa maana tumeyatenda mapenzi yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, naye ametupa amani pande zote.” Basi wakajenga, wakafanikiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akawaambia Yuda, “Tuijenge hii miji na tuizungushie kuta, pamoja na minara, malango na makomeo. Nchi bado ni yetu, kwa sababu tumemtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, tulimtafuta naye ametupatia amani kila upande.” Hivyo wakajenga na wakafanikiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akawaambia Yuda, Na tuijenge miji hii, na kuizungushia maboma, na minara, na malango, na makomeo; nchi bado ikalipo mbele yetu, kwa kuwa tumemtafuta Bwana, Mungu wetu; naam, tumemtafuta, naye amemstarehesha pande zote. Basi wakajenga, wakafanikiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akawaambia watu wa Yuda, “Na tuiimarishe miji kwa kuizungushia kuta na minara na malango yenye makomeo. Nchi bado imo mikononi mwetu kwa maana tumeyatenda mapenzi yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, naye ametupa amani pande zote.” Basi wakajenga, wakafanikiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akawaambia Yuda, “Tuijenge hii miji na tuizungushie kuta, pamoja na minara, malango na makomeo. Nchi bado ni yetu, kwa sababu tumemtafuta BWANA Mungu wetu, tulimtafuta naye ametupa raha kila upande.” Hivyo wakajenga na wakafanikiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akawaambia Yuda, “Tuijenge hii miji na tuizungushie kuta, pamoja na minara, malango na makomeo. Nchi bado ni yetu, kwa sababu tumemtafuta bwana Mwenyezi Mungu wetu, tulimtafuta naye ametupa raha kila upande.” Hivyo wakajenga na wakafanikiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akawaambia Yuda, Na tuijenge miji hii, na kuizungushia maboma, na minara, na malango, na makomeo; nchi bado ingali ipo mbele yetu, kwa kuwa tumemtafuta BWANA, Mungu wetu; naam, tumemtafuta, naye ametustarehesha pande zote. Basi wakajenga, wakafanikiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akawaambia watu wa Yuda, “Na tuiimarishe miji kwa kuizungushia kuta na minara na malango yenye makomeo. Nchi bado imo mikononi mwetu kwa maana tumeyatenda mapenzi yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, naye ametupa amani pande zote.” Basi wakajenga, wakafanikiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo aliwaambia Wayuda: Na tuijenge miji hii na kuizungushia maboma na minara na kutia humo malango yenye makomeo; nchi hii ingaliko wazi mbele yetu, kwani tumemtafuta Bwana Mungu wetu; naye kwa hivyo, tulivyomtafuta, ametupatia kutulia pande zote. Basi, wakaijenga, wakafanikiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akawaambia Yuda, Na tuijenge miji hii, na kuizungushia maboma, na minara, na malango, na makomeo; nchi bado ikalipo mbele yetu, kwa kuwa tumemtafuta BWANA, Mungu wetu; naam, tumemtafuta, naye amemstarehesha pande zote. Basi wakajenga, wakafanikiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Asa alikuwa na jeshi la waaskari elfu mia tatu kutoka Yuda, wenye ngao na mikuki, na wengine elfu mia mbili na makumi nane kutoka katika kabila la Benjamina, wenye ngao na pinde. Wote walikuwa watu mashujaa sana.