2 Chronicles 15:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Asa alimwondoa hata Maaka, mama yake, katika cheo chake cha mama malkia, kwa sababu alitengeneza sanamu ya kuchukiza ya Ashera, mungu wa kike. Asa alikatilia mbali sanamu hiyo, akaipondaponda na kuiteketeza katika bonde la kijito Kidroni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme Asa akamwondolea Maaka, bibi yake, wadhifa wake kama mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo, akaivunjavunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata na Maaka mamaye Asa, mfalme akamwondolea daraja yake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake, akaiponda, akaiteketeza penye kijito cha Kidroni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Asa alimwondoa hata Maaka, mama yake, katika cheo chake cha mama malkia, kwa sababu alitengeneza sanamu ya kuchukiza ya Ashera, mungu wa kike. Asa alikatilia mbali sanamu hiyo, akaipondaponda na kuiteketeza katika bonde la kijito Kidroni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme Asa akamwondolea Maaka mama yake wadhifa wake asiwe mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza kichakani nguzo ya chukizo ya Ashera. Asa akaikata ile nguzo akaiangusha, akaivunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Asa akamwondolea Maaka mama yake wadhifa wake kama mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo, akaivunjavunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata na Maaka mamaye Asa, mfalme akamwondolea cheo chake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake, akaiponda, akaiteketeza penye kijito cha Kidroni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Asa alimwondoa hata Maaka, mama yake, katika cheo chake cha mama malkia, kwa sababu alitengeneza sanamu ya kuchukiza ya Ashera, mungu wa kike. Asa alikatilia mbali sanamu hiyo, akaipondaponda na kuiteketeza katika bonde la kijito Kidroni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme Asa akamwondoa naye mama yake Maka katika ukuu wake, kwa kuwa alitengeneza kinyago cha Ashera, nacho kinyago chake Asa akakikatakata na kukipondaponda, kisha akakiteketeza penye kijito cha Kidoroni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata na Maaka mamaye Asa, mfalme akamwondolea daraja yake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake, akaiponda, akaiteketeza penye kijito cha Kidroni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Asa alimwondoa hata mama yake Maka, cheo chake cha malkia, kwa sababu alitengeneza sanamu ya kuchukiza ya Ashera, mungu wa kike. Asa alikatakata sanamu hiyo, akaipondaponda na kuiteketeza kwa moto katika bonde la kijito Kidroni.