2 Chronicles 15:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asa alipoyasikia maneno haya, yaani unabii wa Azaria mwana wa Odedi, alipata moyo. Akaziondoa sanamu zote za kuchukiza katika nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka katika miji yote aliyoiteka katika nchi ya milima ya Efraimu. Pia, akaitengeneza upya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu iliyokuwa katika ukumbi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi yule nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka miji aliyoiteka katika nchi ya vilima ya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Asa alipoyasikia maneno hayo, yaani, unabii wa mwana wa Odedi nabii, akatiwa nguvu, akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi ya Yuda na Benyamini, na katika miji aliyoitwaa milimani mwa Efraimu; akaifanyiza tena madhabahu ya Bwana, iliyokuwako mbele ya ukumbi wa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asa alipoyasikia maneno haya, yaani unabii wa Azaria mwana wa Odedi, alipata moyo. Akaziondoa sanamu zote za kuchukiza katika nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka katika miji yote aliyoiteka katika nchi ya milima ya Efraimu. Pia, akaitengeneza upya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu iliyokuwa katika ukumbi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Obedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka katika miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya BWANA iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya bwana iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Asa alipoyasikia maneno hayo, yaani, unabii wa mwana wa Odedi nabii, akatiwa nguvu, akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi ya Yuda na Benyamini, na katika miji aliyoitwaa milimani mwa Efraimu; akaitengeneza upya madhabahu ya BWANA, iliyokuwako mbele ya ukumbi wa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asa alipoyasikia maneno haya, yaani unabii wa Azaria mwana wa Odedi, alipata moyo. Akaziondoa sanamu zote za kuchukiza katika nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka katika miji yote aliyoiteka katika nchi ya milima ya Efraimu. Pia, akaitengeneza upya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu iliyokuwa katika ukumbi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asa alipoyasikia hayo maneno ya ufumbuaji wa mfumbuaji Odedi akajishupaza, akayatowesha matapisho katika nchi yote ya Yuda na ya Benyamini, hata katika miji, aliyoiteka milimani kwa Efuraimu, nayo meza ya kumtambikia Bwana iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Bwana akairudishia upya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Asa alipoyasikia maneno hayo, yaani, unabii wa mwana wa Odedi nabii, akatiwa nguvu, akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi ya Yuda na Benyamini, na katika miji aliyoitwaa milimani mwa Efraimu; akaifanyiza tena madhabahu ya BWANA, iliyokuwako mbele ya ukumbi wa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Asa aliposikia maneno haya, ni kusema unabii wa Azaria mwana wa Odedi, yakamutia moyo. Akaondoa sanamu zote za kuchukiza katika inchi yote ya Yuda na ya Benjamina, na kutoka katika miji yote aliyoteka katika inchi ya milima ya Efuraimu. Na kisha akatengeneza upya mazabahu ya Yawe iliyokuwa katika baraza la nyumba ya Yawe.