2 Chronicles 15:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asa aliwaita watu wote wa Yuda na Benyamini, na wengine wote waliokuwa wakikaa nchini mwake kutoka Efraimu, Manase na Simeoni. Hawa walikuja kwake walipoona kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni walioishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba Mwenyezi Mungu, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu, na wa Manase, na wa Simeoni; kwa kuwa walimwangukia wengi katika Israeli, walipoona kwamba Bwana, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asa aliwaita watu wote wa Yuda na Benyamini, na wengine wote waliokuwa wakikaa nchini mwake kutoka Efraimu, Manase na Simeoni. Hawa walikuja kwake walipoona kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni waliokuwa wanaishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba BWANA Mungu wake alikuwa pamoja naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni waliokuwa wanaishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba bwana Mwenyezi Mungu wake alikuwa pamoja naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu, na wa Manase, na wa Simeoni; kwa kuwa walimjia wengi katika Israeli, walipoona kwamba BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asa aliwaita watu wote wa Yuda na Benyamini, na wengine wote waliokuwa wakikaa nchini mwake kutoka Efraimu, Manase na Simeoni. Hawa walikuja kwake walipoona kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawakusanya Wayuda na Wabenyamini wote nao waliokaa ugenini kwake, Waefuraimu na Wamanase na Wasimeoni, kwani wengi waliokuwa Waisiraeli walirudi upande wake walipoona, ya kuwa Bwana Mungu wake yuko pamoja naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu, na wa Manase, na wa Simeoni; kwa kuwa walimwangukia wengi katika Israeli, walipoona kwamba BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Asa akakusanya watu wote wa Yuda na Benjamina, na wengine wote waliokuwa wakikaa katika inchi yake kutoka kabila la Efuraimu, la Manase na la Simeoni. Hawa walikuja kwake walipoona kwamba Yawe, Mungu wake yuko pamoja naye.