2 Chronicles 16:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa mfalme Asa, Baasha, mfalme wa Israeli, aliishambulia nchi ya Yuda na kuanza kuujenga mji wa Rama ili apate kuzuia mtu yeyote asitoke wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa Asa, Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwake Asa, Baasha mfalme wa Israeli akapanda juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu ye yote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa mfalme Asa, Baasha, mfalme wa Israeli, aliishambulia nchi ya Yuda na kuanza kuujenga mji wa Rama ili apate kuzuia mtu yeyote asitoke wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwa Asa, Mfalme Baasha wa Israeli akaishambulia Yuda na kuujengea ngome mji wa Rama ili kumzuia ye yote asitoke wala kuingia katika nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa Asa, Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwake Asa, Baasha mfalme wa Israeli alipanda dhidi ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu yeyote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa mfalme Asa, Baasha, mfalme wa Israeli, aliishambulia nchi ya Yuda na kuanza kuujenga mji wa Rama ili apate kuzuia mtu yeyote asitoke wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa 36 wa ufalme wa Asa ndipo, Basa, mfalme wa Waisiraeli, alipopanda kuijia nchi ya Yuda, akajenga Rama, asipatikane mtu anayeweza kutoka wala kuingia kwa Asa, mfalme wa Wayuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwake Asa, Baasha mfalme wa Israeli akapanda juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu ye yote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa makumi tatu na sita wa utawala wa mufalme Asa, Basha, mufalme wa Israeli, alishambulia inchi ya Yuda na kuanza kujenga muji wa Rama kusudi apate kuzuia mutu yeyote asitoke wala asiingie kwa Asa, mufalme wa Yuda.