2 Chronicles 16:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maneno haya yalimfanya Asa amkasirikie sana Hanani mwonaji, hata akamfunga gerezani. Wakati huohuo, Asa alianza kuwatesa vikali baadhi ya watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asa akamkasirikia mwonaji kwa sababu ya jambo hili. Alikuwa ameghadhibika sana hata akamweka gerezani. Wakati huo huo Asa akaanza kuwatesa na kuwaonea baadhi ya watu kwa ukatili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Asa akamkasirikia mwonaji, akamtia nyumbani mwa mkatale; maana amemghadhibikia kwa sababu ya neno hilo. Na Asa akawaonea baadhi ya watu wakati ule ule.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maneno haya yalimfanya Asa amkasirikie sana Hanani mwonaji, hata akamfunga gerezani. Wakati huohuo, Asa alianza kuwatesa vikali baadhi ya watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asa akamkasirikia mwonaji kwa sababu ya jambo hili. Alikuwa ameghadhibika sana hata akamweka gerezani. Wakati huo huo Asa akaanza kuwatesa na kuwaonea baadhi ya watu kwa ukatili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asa akamkasirikia mwonaji kwa sababu ya jambo hili. Alikuwa ameghadhibika sana hata akamweka gerezani. Wakati huo huo Asa akaanza kuwatesa na kuwaonea baadhi ya watu kwa ukatili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Asa akamkasirikia mwonaji, akamtia katika nyumba ya mkatale gerezani, maana amemghadhibikia kwa sababu ya neno hilo. Na wakati uleule Asa akatesa baadhi ya watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maneno haya yalimfanya Asa amkasirikie sana Hanani mwonaji, hata akamfunga gerezani. Wakati huohuo, Asa alianza kuwatesa vikali baadhi ya watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asa akamkasirikia mtazamaji, akamfunga nyumbani mwenye mikatale, kwani alimchafukia kwa ajili ya hayo. Nao watu wengine Asa akawakorofisha siku zile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Asa akamkasirikia mwonaji, akamtia nyumbani mwa mkatale; maana amemghadhibikia kwa sababu ya neno hilo. Na Asa akawaonea baadhi ya watu wakati ule ule.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Asa akamukasirikia sana nabii Hanani, hata akamuweka katika kifungo; maana amekuwa na hasira kubwa naye juu ya maneno yale. Wakati uleule, Asa akaanza kuwatesa vikali wamoja kati ya watu.